"Tulichukua njia ya mkato kuelekea nyumbani. Sikuona
dalili zozote kuwa Maria anamtambua Idda, nami
nikajipongeza... "Willy niliiweka roho yangu mikononi
mwako nilipoamua kuishi nawe, lakini kwa sababu
umeshindwa kuitunza vizuri nimeamua kuirudisha."
Laiti mtu angelijua harufu ya mauti yake basi angeyakimbia
kila yanapotaka kumfikia. Lakini kwa kuwa
mwanadamu hatambui kuwa matendo yake na
mwelekeo wa maisha ndiyo huwa harufu ya mauti
yake, hujikuta amenaswa na mauti bila kutarajia.