Omschrijving
Baada ya kufanya vizuri katika mtihani, Sudi na Shada wanapelekwa nawazazi wao kwenye mbuga ya wanyama. Wanapofika mbugani, Sudianatoweka pasi na yeyote kumwona. Wazazi wake na dada yakewanaanza kumtafuta. Je, Sudi anapatikana?Hadithi Mufti za Longhorn ni mfululizo mpya wa hadithi ambazozimeandikwa kulingana na mtaala mpya. Hizi hadithi zinalenga kukuzaujuzi wa wanafunzi kupitia kwa uvumbuzi wa maarifa na zinaimarishauelewa wao wa masuala ibuka katika jamii. Hadithi hizi sio tu za kuelimishana kuburudisha, bali pia zimeambatanishwa na mazoezi ambayoyatawasaidia wanafunzi kuimarika kiubunifu, kimawazo na kifikra.